MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imelemewa na umati wa watu wanaojitokeza kulipia kodi ya majengo na kusababisha misururu kuwa mirefu zaidi katika vituo vya mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Hali hiyo imefanya baadhi ya watumishi walioajiriwa maofisini kushindwa kulipa kodi hiyo, kwa kuwa muda wa kukaa mtu kwenye foleni unachukua kutwa nzima, ambapo watumishi wengi wa maofisini walishindwa kuvumilia na kulazimika kurudi maeneo yao ya kazi.
Tangu TRA iongeze muda baadhi ya vituo vya mamlaka hiyo vimeendelea kuwa na misururu mirefu ya watu, jambo linaloonesha kuwa bado maelfu ya watu hawajalipa kodi hiyo ambayo mwaka huu imeitikiwa na wananchi wengi toafuti na miaka ya nyuma.
“Jana (juzi) nilikuja hapa saa nne asubuhi, lakini sikufanikiwa kulipa kodi kwani msururu ulikuwa mrefu, leo nimeamka alfajiri lakini sina uhakika kama nitaingia huko ndani,” alisema mwananchi mmoja aliyekuwa katika ofisi ya TRA Vingunguti. Watu katika kituo hicho waliomba kuongezwa watumishi wa TRA ili iwe rahisi kushughulikia umati mkubwa huo wa watu.
Katika ofisi hizo hali ilikuwa ya kutisha na baadhi ya watu waliofika eneo hilo kuanzia saa nne asubuhi walilazimika kugeuza kutokana na kukata tamaa ya vurugu zilizokuwepo. Mwandishi wa gazeti hili ambaye pia alifika katika ofisi za TRA Kimara alishuhudia umati mkubwa wa watu ukiwa unasubiri kuingia ndani ili kulipia kodi ya majengo.
“Hapa Kimara hali ni mbaya sana, kuna umati mkubwa wa watu na wengi wamekata tamaa ya kulipa kodi, wamegeuza,” alisema mkazi wa Kibamba, Stella Nyoni. Licha ya TRA kulegeza masharti ya kuwataka wananchi waende moja kwa moja ofisi za TRA kuchukua fomu na kujaza na kulipa moja kwa moja, lakini bado utaratibu huo haukusaidia kupunguza umati wa watu.
Wakati hali ikiwa hivyo, Kituo cha Kodi cha Buguruni Dar es Salaam kimesema kinatoa huduma hadi usiku wa saa 4. Kwa mujibu wa baadhi ya walipa kodi ya majengo waliokutwa na gazeti hili wakiwa kwenye foleni kwa ajili ya kufanya malipo hayo kwenye kituo hicho kilichopo Vingunguti jijini humo, ambao hata hivyo hawakutaka kutajwa majina, walisema awali huduma ilikuwa ikitolewa hadi saa 11:00 jioni.
Walisema kwa nyakati tofauti kuwa, kusitishwa kwa huduma hiyo saa 11:00 jioni kwa siku, kuliwasababisha walioshindwa kuhudumiwa kutokana na ufinyu wa muda, kurejea siku iliyofuata na kujikuta wakikaa kwenye foleni kwa muda mrefu kabla ya kuhudumiwa.
Ofisa Msimamizi wa kituo hicho cha kodi cha Vingunguti ambaye hakutaka kutajwa pia kwa maelezo kuwa si msemaji wa mamlaka hiyo, alisema tangu muda wa wiki mbili ulipoongezwa kuwapa muda ambao hawajalipa kodi ya majengo wafanye hivyo, wamekuwa wakihudumia wateja hadi usiku wa saa nne.
“Tunahudumia hadi saa 3 au saa 4 usiku, kulingana na wingi wa wateja waliotufikia. Tulichoamua ni kuhakikisha waliopo kwenye foleni hawarudi nyumbani bila kupata huduma,” alisema ofisa huyo.
Aliongeza kuwa kwa siku wanahudumia wastani wa walipa kodi 800 na kwamba waliongeza wahudumu wa kushughulika na wanaolipa kodi hiyo ili kuendana na muda. Akizungumzia siku ya kesho iliyobaki ili Watanzania ambao hadi sasa hawajalipa kodi hiyo ya majengo wafanye hivyo, Msimamizi huyo alisema wasipoteze muda kwenda kutafuta fomu za usajili wa majengo Serikali za Mitaa.
Aliwashauri wazipakue kutoka kwenye mtandao wa mamlaka hiyo (www.tra. go.tz) kuzijaza na kuziwasilisha kwenye vituo husika vya kodi zikiwa zimejazwa vyema. Kwa upande wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF) kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, watu walizidi kuongezeka katika banda la TRA jana kwa ajili ya kulipia kodi ya majengo. Gazeti hili limeshuhudia
0 Maoni:
Post a Comment