Wanaume wawili wanatarajiwa kupokea
adhabu ya viboko katika mkoa wa Acheh nchini Indonesia baada ya
kupatikana na hatia ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Wawili hao watapokea viboko 85 kila mmoja adhabu ikitolewa mbele ya umma
Wanaume hao wa miaka 20 na 23 walifumaniwa wakiwa ndani ya kitanda na makundi ya sungusungu yaliyovamia makaazi yao mwezi machi.
Kabla ya kufumaniwa na kundi la sungu sungu mmoja wao alikuwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu akisomea udaktari.
Aliwaambia waandishi wa habari kuwa mipango yake ilikuw akuwe daktari. Kwa sasa inaripotiwa kuwa chuo alichokuwa akisomea kimemtimua.
Video za wawili hao wakifumania zilisambazwa kwa wingi kwenye mitandao ya kijamii wakiwa wote uchi huku wakiomba msaada.
Sheria kali dhidi ya mapenizi ya jinsia moja zilipitioshwa mwaka 2014 na kuanza kutekelezwa mwaka uliofuatia.
Hukumu za kuchapwa viboko zimetolewa awali kwa makosa yanahusu kucheza kamari na unywaji pombe.
0 Maoni:
Post a Comment