Arusha. Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amesema wamekamilisha safari ya kuwapeleka Marekani majeruhi watatu wa ajali iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa Shule ya Lucky Vincent ya Arusha.
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
Akizungumza leo (Alhamisi) katika ofisi ya mganga mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, Nyalandu amesema ndege maalumu ya kuwabeba majeruhi hao imetolewa na Shirika la Samaritan Fund la nchini Marekani ambayo itawasili LEO
Nyalandu amesema rubani anatarajiwa kuwasili jijini Arusha JANA akitokea Nairobi nchini Kenya na iwapo kila kitu kitakamilika safari itakuwa Jumamosi.
"Watakaoondoka ni abiria wanane, ambao ni majeruhi na wazazi wao, muuguzi mmoja na daktari mmoja. Hati za kusafiria ziko tayari, kinachosubiriwa ni viza," amesema Nyalandu.
0 Maoni:
Post a Comment