
Michuano ya kombe la dunia la vijana
chini ya umri wa miaka 20 inaendelea kushika kasi huko nchini Korea ya
kusini ikiwa katika ngazi ya makundi.
Kwenye kundi D Afrika ya kusini walichapwa na Italia kwa mabao 2-0, huku Uruguay wakiwafunga Japani kwa 2-0.

Kikosi cha timu ya taifa ya Uruguay
Michuano hiyo inaendelea tena leo katika kundi E Ufaransa watacheza na Vietnam, na New Zealand wakipepetana na Honduras.
Katika kundi F Ecuador wataonyesha ubavu na Saudi Arabia, huku Senegal wakicheza na Marekani.
0 Maoni:
Post a Comment