Mahakama kuamua kuhusu kura dhidi ya rais Zuma

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini
Mahakama ya kikatiba nchini Afrika Kusini inatarajiwa kuamua kuhusu iwapo wabunge wanaweza kupiga kura ya siri ya kutokuwa na imani na rais Jacob Zuma au la.
Hatua hiyo inajiri kufuatia hali ya switofahamu kuhusu uongozi wa Bwana Zuma huku kukiwa na madai ya uajiri wa marafikize serikalini na ufisadi.
Bwana Zuma hivi majuzi alimewa katika baadhi ya mikutano ya hadhara huku maafisa wakuu wa chama chake wakionekana hadharini kujipigia debe ili kumrithi kiongozi huyo kama kiongozi wa chama.
Upinzani unadai kwamba wabunge wanastahili kuongozwa imani yao na sio uongozi wa vyama vyao kwa kuwa uongozi wa rais Zuma ni swala mushimu la kitaifa.
Hatua hiyo ya kupiga kura ya kutokuwa na imani naye ilisababishwa na kumfuta kazi waziri wa fedha na naibu wake miezi miwili iliopita.
Hatua hiyo ilifanya uwezo wa kifedha wa taifa hilo kushuka.
Hatahivyo nbaadhi ya wachanguzi wanaamini kwamba hata iwapo mahakama ya kikatiba itawapatia wabunge haki ya kupiga kura kwa siri, wanachama wengi wa ANC watamuunga mkono kiongozi.
Kama alivyosema mbunge mmoja, hataki kufuata wito wa upinzani na kwamba atakabili swala la bwana Zuma kama la ndani ya chama.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment