Mkwe wa rais Donald Trump na mshauri
mkuu Jared Kushner anachunguzwa na shirika la FBI ikiwa ni miongoni mwa
uchunguzi wa Urusi kulingana na vyombo vya habari nchini Marekani.
FBI linachunguza hatua ya Urusi kuingilia uchaguzi wa urais wa 2016 nchini humo na ushirikiano wa kundi la kampeni la rais Trump.
Rais Trump amekana madai yoyote ya kujihusisha na Urusi wakati wa kampeni.
Wakili wa bwana Kushner amesema kuwa mteja wake atashirikiana na wachunguzi hao kuhusu uchunguzi wowote.
Rais Trump ametaja hali hiyo kuwa 'uwindaji' mkubwa wa kiongozi katika historia ya Marekani.
Vitengo vya ujasusi vinaamini Moscow ilijaribu kukisaidia chama cha Republican kushinda uchaguzi huo dhidi ya mgombea wa chama cha Democrat Hillary Clinton.
Maafisa wa Marekani waliotajwa waliambia chombo cha habari cha NBC kwamba hatua ya kumchunguza bwana Kushner mwenye umri wa miaka 36 haimaanishi kwamba wachunguzi wanamshuku kuhusu uhalifu fulani na kwamba wanataka kumshtaki.
Kwengine ,gazeti la Washington Post limeripoti kwamba wachunguzi hao walikuwa wakiangazia mikutano aliofanya mwaka uliopita na balozi wa Urusi nchini Marekani ,Sergei Kislyak na mfanyikazi mmoja wa benki kutoka Moscow.
0 Maoni:
Post a Comment