Chama cha Wamiliki wa Mabasi nchini (TABOA) kwa kushirikiana na Chama
cha Wasafirishaji Mkoa wa Dar es Salaam kimetangaza mgomo wa
usafirishaji abiria na mizigo nchi nzima ili kushinikiza Serikali
kutopitisha sheria ya usafirishaji inayotarajiwa kupitishwa siku ya
Jumanne.
Mgomo huo utaanza leo Jumatatu.
Uamuzi huo umefikiwa katika Mkutano Mkuu Maalum wa TABOA ambapo Katibu
Mkuu, Eneo Mrutu amesema sheria hiyo mpya inayotarajiwa kupitishwa
haikuwashirikisha wadau na haitenganishi makosa ya dereva na mmiliki wa
chombo cha usafirishaji na kupelekea mmiliki kufungwa jela.
Mrutu amewataka wabunge bila kujali itikadi zao kutopitisha sheria hiyo
hadi itakapobadilishwa na kushirikisha wadau kwakuwa inalenga kuharibu
sekta ya usafirishaji nchini.
0 Maoni:
Post a Comment