FAMILIA ya mzee John Mbembela katika kijiji na kata ya
katete wilaya ya kalambo mkoani Rukwa imenusurika kifo
baada ya kupata ajari ya kufukiwa na vipande vya matofari ya
kuchoma yalio tokana na kuanguka kwa nyumba yao kufuatia
kujitokeza kwa tetemeko la aridhi na kupelekea kukosa mahali pa
kuishi na huku serikali wilayani humo ikingilia kati saka hilo.
Tetemeko la aridhi katika wilaya ya kalambo mkoani Hapa
lilipita usiku wa kuamkia February 24 majira ya saa tisa na
nusu usuku , ambapo kufuatia tetemeko hilo kujitokeza familia
ya john mbembela katika kijiji na kata ya katete ilijikuta
kwenye wakati mgumu baada ya kufukiwa na vipande vya matofali ya
kuchoma kufuatia kuangukiwa na nyumba yao ilio sabishwa na
tetemeko la aridhi na kujitokeza kwa nyufa kwenye nyumba za watu
wengine na kufanya serikali wilayani humo kupitia ofis ya mkuu
wa wilaya kuingilia kati sakata hilo sambamba na kuwakimbiza
wathirika wa tukio hilo kwenye kituo cha afya matai kwa matibabu.
Wathirika wa tukio hilo akiwemo mzee John Mbembela wamekiela
kituo hiki kuwa chanzo ni baada ya kujitokeza kwa tetemeko la
aridhi ambalo lilisabisha nyumba yao kuwangukia kisha kupata
majeraha katika sehemu mbalimbali za mili yao na huku wakiomba
serikali kuwangalia kwa jicho la tatu kutokana na kukosa mahali
pa kuishi.
Mtendaji wa kijiji hicho primo Nyami ambae licha ya kukili
kutokea tukio hilo,amesema tetemeko hilo limeathiri makazi ya
watu na kuweka nyufa kwa baadhi ya nyumba kijijini hapo.
Kaimu mganga mkuu wa wilaya hiyo Tuse Kasanga , ambae licha ya
kuli kuwapokea wagonjwa hao , amesema kwasasa wanaendelea vizuri .
Katibu tawala wa wilaya hiyo Frank Schalo , amba licha ya kuli
kuwepo adha hiyo, amewata wananchi kukimbilia nje pindi
tatizo kama hilo linapotokea ili kuepukana na kuangukiwa na
nyumba zao.
0 Maoni:
Post a Comment