Manchester United wameafikia
makubaliano ya kumsaini mlinzi raia wa Sweden Victor Lindelof kutoka
Benfica kwa kima cha pauni milioni 31.
Lindelof, ambaye ameichezea nchi yake mara 12 anatarajiwa kushiriki mechi ya kirafiki nchini Norway siku ya Jumanne
Mchezaji huyo mwenye maiak 22 ambaye amekuwa akiichezea Benfica tangu mwaka 2012 atakuwa mchezaji wa kwanza kusainiwa na Man U msimu huu.
Lindelof alicheza mara 47 klabu hiyo ya Ureno msimu uliopita.
0 Maoni:
Post a Comment